Kiwango kikubwa cha theluji
iliyoanguka imesababisha kuvurugika kwa shughuli za usafiri na utaratibu
wa shule nchini Uingereza, huku mvua kubwa ikinyesha na kuleta mafuriko
kusini magharibi mwa England.
Vikundi vya uokoaji vinamtafuta mwananmke mmoja
katika nyumba moja ambayo imeanguka upande kutokana na maporomoko ya
ardhi huko Looe, Cornwall.Kuna taarifa 18 zilizotolewa zikitahadharisha kuwepo kwa mafuriko Kusini Magharibi, huku Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa ikionya kuanguka theluji zaidi katika maeneo mengi ya Uingereza.
Zaidi ya shule 1,000 nchini Uingereza zimefungwa ambapo wateja 50,000 Ireland Kaskazini hawana umeme.
Waandishi wa BBC wa masuala ya hali ya hewa wamesema theluji hiyo itasababisha kuvurugika kwa usafiri katika maeneo ya kaskazini ya Uingereza, siku ya Ijumaa, huku maeneo mengine yakishuhudia theluji kufikia kiwango cha kati ya sentimita 20-40.
Barabara katika maeneo ya kaskazini mwa Wales, Midlands huko Pennines, kusini mwa Scotland na Ireland Kaskazini yataathiriwa vibaya kutokana na theluji hiyo, wakati upepo mkali utapeperusha theluji hiyo na kupita katika mkondo wa njia za eneo la Pennine, wamesema.
chanzo: bbc
0 comments:
Post a Comment