pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Wasanii Kenya wamlilia E Sir




 

 
Nairobi, Kenya
.Wasanii mbalimbali nchini Kenya, wikiendi hii walitumia mitandao ya jamii kumkumbuka mmoja wa wasanii ambae anatajwa kama mwasisi wa muziki wa Genge marehemu Issah Mmari au E-Sir ambaye siku ya Jumamosi alikuwa anatimiza miaka 10 tangu afariki dunia.
E Sir alikuwa ni kati ya wasanii wa mwanzo nchini Kenya kurapu kwa lugha ya Kiswahili.
Siku ya Jumamosi wasanii tofauti tofauti waliandika kwenye mitandao yao juu ya msanii huyo aliyefari, au ki tarehe 16 March mwaka 2003 kwa ajali ya gari akiwa anatoka kufanya onyesho nchini Nakuru kwa ajili ya kuitangaza albumu yake ya kwanza na ya mwisho pia.
Baadhi ya wasanii kama Wahu ambaye ni mke wa msanii Nameless aliandika kwa lugha ya Kiingereza, “Ni miaka 10 tangu tupoteze moja ya watu muhimu katika soko la muziki wa Kenya, lakini ingawaje hayupo na sisi kimwili lakini bado tunaishi nae kupitia kazi zake alizoziacha, E Sir tunakukumbuka, uendelee kupumzika kwa amani”,

CHANZO: MWANANCHI

































































0 comments:

Post a Comment