pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Wasichana wadogo wafanya biashara ya ngono


 
Ni usiku wa saa 4 nipo katika eneo maarufu la Buguruni lililopo jijini Dar es Salaam nikiwa nimekaa napata kinywaji kwenye baa moja.

Katika eneo hilo ambalo lipo pembezoni mwa Barabara ya Mandela si tulivu sana kutokana na pilika pilika za magari na watu wanaopita karibu kwa shughuli mbalimbali.
Huku nikiendelea kupata kinywaji mara naona wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wakizunguka zunguka katika eneo hili la baa.

Awali nilifikiri walikuwa wakitafuta msaada au wakipita kuelekea nyumbani kwao, kwani umri wao haukunipa picha kwamba walikuwa kazini wakati huo wa usiku wa kiza kinene.
Kilichonifanya niwaangalie kwa udadisi zaidi ni kuona jinsi walivyovaa nguo ambazo zilionyesha nusu ya sehemu zao za mapaja, huku kifuani wakiwa wamevaa blauzi zilizobana zikionyesha matiti yao madogo ambayo yanaanza kuchipua.

Kilichonitisha zaidi ni kuona wasichana hawa ambao wakati huo walipaswa kuwa nyumbani wakiwa mkononi wameshika vinywaji vikali aina ya ‘viroba’ na wengine wakivuta sigara.
Hawa ni sehemu ndogo tu ya wasichana wadogo ambao hukesha usiku kucha katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakitafuta wateja ili wapate fedha za kujikimu.
Mwandishi analazimika kuwadadisi wasichana hawa ili kujua nini kilichosababisha waingie katika biashara hii.

Inavyokuwa
Mwandishi ana mwita mmoja wa wasichana hawa Neema Mashiri (16) (sio jina lake halisi) na kuongea naye katika sehemu tulivu katika baa hiyo huku wakitumia vinywaji kunogesha mazungumzo.

Neema akiwa mwenye kujiamini na kazi yake bila ya kutetereka anasema kazi hiyo aliianza zaidi ya miezi sita nyuma huku akiwa tayari amekutana na idadi ya wanaume ambayo haikumbuki kutokana na wingi wake.

“Kwa siku moja nakutana na wanaume katiya watano hadi saba na hii hutegemea siku na siku, kwani kuna siku huwa na biashara ya kutosha na tunapata fedha za kutosha,” anasema Neema.

Neema akieleza ujira ambao hulipwa anasema ni Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa muda usiozidi dakika 30 kwa mwanamume mmoja huku wakati kwa yule anayetaka kulala naye hadi asubuhi hutakiwa kulipa Sh10,000 hadi Sh15,000.

“Baadhi ya wanaume wamekuwa wakitufanyia vitendo vya kikatili kwa kutuingilia kinyume cha maumbile, lakini kutokana na hali ngumu ya maisha hukubali kwani dau huwa kubwa Sh10,000 hadi Sh12,000, lakini wengine hutumia ubabe tu na kututumia bila kutulipa,” anasema Neema na kuongeza;

Neema alizaliwa mkoani Arusha eneo la Sakina na kusoma katika Shule ya Sekondari Usa na kuishia kidato cha pili kutokana na kuugua kila alipoingia darasani.

Kitu gani kilichosababisha Neema aje Dar na kufanya biashara hiyo?
Anasema ni kutokana na ugomvi baina ya baba na mama yake ambao walikuwa wakikorofishana mara kwa mara kwa sababu mama yake alidai kuwa bibi mzaa baba wa Neema ni mchawi na ndiye aliyemroga Neema na kumsababisha augue kila anapoingia darasani.

Neema anasema hatimaye mama na baba yake waliachana na yeye na mama yake wakaja Dar es Salaam na kuishi maeneo ya Tabata Reli.
Naye Sikitu Alfred (15) mzaliwa wa Mbeya anasema anaifanya kazi hiyo kutokana na ugumu wa maisha na hana njia nyingine ya kujiingizia kipato.

Anasema ameanza kazi hiyo mwishoni mwa mwaka 2011 alipokuwa anaishi na shangazi yake Vingunguti na huko alikuwa akikutana na vijana mtaani kwao.

Aliongeza kuwa alipoanza biashara hiyo hali yake ilianza kubadilika, kwani wateja walikuwa wengi kutokana na wanaojiuza kama yeye kuwa wachache, lakini sasa wanaojiuza nao wamekuwa wengi.

Rena yeye anafurahia
Kwa upande wake Rena Robert (15) anasema huwa anafurahia kazi hiyo kutokana na kujiingizia kipato cha kutosha kwa siku.
“Unajua kwa siku moja hukusanya Sh50,000 hizo si pesa kidogo, sidhani kama kazi hii naweza kuiacha kwani ina kila aina ya starehe,” anasema Rena.



Anasema mara ya kwanza kuingiliwa kinyume cha maumbile alijisikia maumivu, lakini aliporudia tena kitendo hicho na ukilinganisha na gharama yake kuwa kubwa hawezi kuacha.
“Hapa dau huwa kubwa kwani kwa mwanamume mmoja tu kuniingilia kinyume cha maumbile ni Sh15,000 na hii ni muda mfupi,” hivyo nikitembea na watatu ninakuwa na fedha za kutosha,” anasema Rena. Wakati hayo yakiendelea Buguruni, katika maeneo ya Manzese Mburahati, Uwanja wa Fisi karibu na kumbi za starehe wakati wa usiku huwezi kukosa kuwaona wasichana wadogo wenye umri kati ya miaka 13 hadi 14 wakitembea kutafuta wateja wa kufanya nao ngono.

Wanaume wanena
Baadhi ya wanaume wanasema kuwa wamekuwa wakifika kupata huduma kutoka kwa akina dada hao kutokana na kuepuka gharama.
“Unajua ukiwa na msichana wa kudumu na maisha yako yakiwa si mazuri atakusumbua, lakini ukija hapa hakuna tatizo mnakutana siku moja na kuachana kila mtu kivyake,” anasema Samson Frank.

Kauli ya Serikali
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu anakiri kukithiri kwa vitendo hivi na kuahidi kuendelea kuvifanyia kazi.Anasema vitendo hivyo ambavyo vinafanywa na watoto walio chini ya miaka 18 ni makosa ya jinai, hivyo jamii na wadau mbalimbali wanatakiwa kuungana kukomesha vitendo hivi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Minangi anasema wanaendelea na operesheni ya kuwakamata makahaba.
chanzo Mwananchi

0 comments:

Post a Comment