Mchele ni moja ya chakula kinachotumika sana
hapa nchini. Kwenye maduka na masoko hupatikana kwa wingi na inapotokea
kuadimika ama bei yake kupanda, wengi hutaabika na kujikuta katika hali
ngumu ya maisha.
Pamoja na mchele kupendwa, wanunuzi wamekuwa na mitihani mingi wanapoenda kuinunua dukani maana hukuta majina mbalimbali au hupima kwa kuchunguza harufu yake.
Hapa nchini, wanunuzi wengi huzoea kuita michele kwa majina kama vile Morogoro, Kitumbo, VIP, Magugu na Mbeya ambao nao umegawanyika katika makundi kadhaa lakini unaopendwa zaidi ni ule unaotoka Kyela kwa madai ya kuwa na harufu nzuri. Magugu ambao unalimwa Arusha, ni miongoni mwa ile inayopendwa sana na walaji.
Zao hilo linatokana na mpunga na hulimwa kwenye eneo lenye hali ya umajimaji kwa wingi. Ndiyo maana kwa hapa nchini zao hilo humea zaidi maeneo ya uwanda wa chini (mabondeni) ambamo udongo wake huwa katika hali ya umajimaji kwa kipindi kirefu.
Kwenye maduka na masoko hapa nchini waweza kukuta aina sita za mchele lakini wataalamu wa mimea wamebaini zipo aina 235 za mchele duniani na huenda zikaongezeka kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kuwepo kwa aina nyingi za mchele kumesababisha wanasayansi wakae chini wasugue vichwa kubaini chanzo cha mnyumbuliko huo.
Katika hatua ya awali walitumia kipimo cha viwango na aina ya wanga inayopatikana kila aina ya mchele ikilinganishwa pia na uwiano wa kwenye mbegu. Kwa kutumia kipimo cha kitaalamu kinachojulikana kama Glycemic Index (GI) waliweza kubaini kiwango hicho ni cha juu ama cha chini. Hivyo wakabaini tofauti za mchele zinategemea kiwango cha GI kwenye zao husika.
Mchele kuwa na GI tofauti
Jarida maarufu barani Asia linaloandika taarifa za kisayansi lijulikanalo kama AsianScientist toleo la Julai, mwaka jana liliinukuu timu ya watafiti wa Taasisi ya Kimataifa ya zao la Mchele (IRRI) na ile inayojishughulisha na Tafiti za Vyakula (CSIRO), ilichunguza tabia za mchele kubadilika badilika maeneo mbalimbali duniani na kufanya iwe na GI tofauti.
Baada ya utafiti wao, wakabaini aina ya chembe ya uzazi ambayo huwezesha mchele kuwa na GI tofauti. Wakabaini kuwa chembe hiyo huweza kubadilika-badilika kirahisi kulingana na mazingira kwa kusababisha aina fulani ya nta inayoathiri mbegu inayozalishwa na mpunga husika. Kiongozi wa timu iliyoendesha utafiti huo, Profesa Melissa Fitzgerald kutoka IRRI, anasema walibaini kuwa mchele wenye kiwango cha juu cha GI unameng’enywa kirahisi katika tumbo la binadamu. Mara nyingi hii ni ile aina ya mchele ambayo hupendelewa kuliwa na watu wengi.
Anasema ile aina ya mchele yenye kiwango cha chini cha GI inatumia muda mrefu kumeng’enywa tumboni na hivyo ni kiwango kidogo tu huchukuliwa na mwili. Kutokana na ugunduzi huu, mchele huo ukabainika unawafaa wale wenye ugonjwa wa kisukari au wanaotaka kupunguza uzito.
“Kutokana na ugunduzi huu, mchele huo ukabainika unawafaa wale wenye ugonjwa wa kisukari au wanaotaka kupunguza uzito.”

0 comments:
Post a Comment