pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Xi Jinping kusaini mkataba ujenzi wa Bandari Bagamoyo


Rais wa China, Xi Jinping 
hare

Dar es Salaam.
 Rais wa China, Xi Jinping anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku moja, ambapo pamoja na mambo mengine atasaini mikataba 17, kati ya nchi hiyo na Tanzania, ukiwamo wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Ujenzi huo utakaofanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China, utakwenda sambamba na ujenzi wa barabara inayounganisha bandari hiyo na Reli ya Kati na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ujio wa rais huyo aliyechaguliwa wiki mbili zilizopita, utakuwa wa manufaa makubwa kwa Tanzania.

“Mbali na mkataba huo pia tutasaini mikataba wa kidiplomasia. Vilevile, China imefungua soko la Watanzania kuuza tumbaku nchini humo na mkataba wa kuliendeleza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),” alisema Membe.

Waziri huyo alisema kiongozi huyo wa China pia atafungua jengo la kisasa la mikutano la Mwalimu Nyerere.

“Kwa kuwa anakuja Afrika kwa mara ya kwanza huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza, Jinping pia atatoa hotuba yake juu ya msimamo wa China kwa Tanzania na Afrika kwa jumla,” alisena Membe.

chanzo Mwananchi

0 comments:

Post a Comment