Sumbawanga. Mtuhumiwa wa wizi,
Christopher Sanga ‘Chinga’ (30), amefariki dunia katika chumba cha
upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga baada ya
kufyatuliwa risasi na polisi.
Taarifa kutoka hospitalini zinasema mtuhumiwa huyo
alijeruhiwa na risasi iliyompiga kwenye nyonga kisha kutokea katikati
ya makalio na alifariki dunia juzi wakati madaktari wakijitahidi kuokoa
maisha yake.
Pia askari wa Kikosi cha Upelelezi wilayani
Sumbawanga, Rock Mnubi (31) naye anaendelea kutibiwa katika hospitali
hiyo alikolazwa baada ya kujeruhiwa kwa fyekeo kichwani na mtuhumiwa.
Kwa mujibu wa mke wa marehemu, Halima Mlongo (27),
askari polisi watano walifika nyumbani kwake wakiwa wamevaa kiraia,
huku wawili kati yao wakiwa na bunduki kila mmoja.
Alidai kuwa walipofika nyumbani hapo waliianza
kuikagua nyumba hiyo, huku yeye akiwa dukani baadaye walimwamuru
amtafute mume wake, yeye aliingia chumbani na kumweleza mumewe kuwa ana
wageni wanamsubiri nje.
Aliongeza kuwa “Askari hao walipiga teke mara
mbili na mlango ukafunguka kisha marehemu akajihami kwa kumkata na
fyekeo mmoja wa askari hao na mwingine kuoana mwenzake amejeruhiwa,
alimfyatulia mume wangu risasi moja na akaanguka chini huku akivuja damu
nyingi.”
Jirani wa marehemu, James Nkondya ambaye
alishuhudia tukio hilo alisema kuwa askari hao hawakumwarifu hata
mwenyekiti wao wa kitongoji ambaye alifika hapo baada ya askari hao
kumpiga risasi Chinga kisha kuondoka zao.
Ndugu wa marehemu huyo walifika mjini hapa kutoka
Makete, walikataa kuuchukua mwili wa marehemu na kuandamana hadi Kituo
cha Polisi wakitaka kuelezwa sababu ya kifo, huku wakitishia kuwa iwapo
polisi wakiamua kumzika wenyewe watakiona.
Baba mdogo wa marehemu, Damian Mbilinyi alisema
walipofika Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa waliambiwa waonane na Ofisa
Upeleleizi wa Mkoa, Peter Ngusa na kushindwa kuafikiana katika
mazungumzo yao, lakini baada ya kubanana nao polisi walitoa ubani wa
Sh1,000,000 na lita 200 za dizeli kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda
Makete kwa maziko.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob
Mwaruanda a mtuhumiwa alipigwa risasi wakati akipambana na polisi
waliotaka kumkamata kwa wizi.
Mwaruanda alisema askari huyo na wenzake walifika
nyumbani kwa mtuhumiwa huyo mali za Sh2.5 milioni, za Kampuni ya Sumry
Enterprises ya mjini Sumbawanga anaodaiwa kutenda Machi 27.
0 comments:
Post a Comment