pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Tanroads Dar yatishiwa kushtakiwa


Dar es Salaam.  Kampuni ya Usangu General Traders (T) Limited, imetoa siku 30 kwa Wakala wa Barabara (Tanroads),Mkoa wa Dar es Salaam   kutoa sababu za kwa nini isishtakiwe kwa  madai ya kuvuruga utekelezaji wa mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme Tanzania  (Tanesco).
Katika barua yake iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Ibrahim Ismail ,  ilielezwa kwamba Tanroads ilikamata mtambo wake wa kunyayua mizigo mizito (crane), uliokuwa ukielekea kufanya kazi kwenye Kituo cha Tanesco eneo la Mikocheni na kusababisha kazi hiyo kuyumba.
Ismail alidai  crane hiyo ilikamatwa tangu Machi 2, mwaka huu na inashikiliwa na Tanroads bila sababu za msingi hadi sasa jambo ambalo linasababisha hasara kwa kampuni yake  .
“Tungependa kuweka suala hili bayana kwamba gharama zote zitakazosababishwa na ukiukwaji huo  wa sheria zitakuwa juu yenu. Hii ni pamoja na kulipa gharama ya mafuta ya diseli lita 400 na yale ya hydraulic’’ ilisema sehemu ya barua hiyo.
Akijibu  hoja hizo , Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Julius  Ndyamukama  alisema  hakuna  hujuma  katika ukamataji wa mtambo huo bali ni utekelezaji wa sheria .
Ndyamukama  katika barua ya majibu kwa kampuni ya Usangu alisema mtambo huo ulikamatwa kwa kuwa haukuwa na kibali cha kutembea na kwamba  hata dereva  hakuwa na kibali.
Utata huo unaibuka wakati gazeti hili toleo la jana lilichapisha habari iliyomkuu kiongozi wa Chama cha Wasafirishaji kwa njia ya Malori (Tatoa), Elias Lukumay akisema kitendo cha Serikali kutaka mitambo  aina ya Carane iwe na kibali kila inapotoka kinachangia kuchelewa kufika maeneo  kuokoa watu wanaokumbwa na ajali.
Lukumay alisema tatizo la Tanroads kudai vibali vya kutembeza cranes linasababisha hata kuchelewa kusafirisha makontena. Alisema tayari wameshamweleza Waziri wa Uchukuzi Dk Harrisn Mwakyembe ili aweze kuwasiliana na mawaziri wengine kuondoa kero hiyo.
MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment