Naibu
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makala, amewataka
watanzania kuacha ushabiki kama wa Simba na Yanga na badala yake
waishangilie kwa nguvu Azam FC katika mchezo wao wa jumamosi dhidi ya
Barrack Young Controllers ya Liberia .
Akizungumza na Raia Mwema jana Makala alisema Azam imekuwa timu imara na yenye kujituma kuhakikisha watanzania wanapata raha, hivyo hakuna budi kuishangilia na kuipa ushirikiano.
“Tuache ushabiki kama wa Simba na Yanga, siku ya jumamosi tuende kuishangilia Azam kwa nguvu zote, siyo hawa wanawashangilia Waliberia wengine wanawashangilia Azam sote tuwe kitu kimoja,” alisema Makala.
Naye msemaji wa Azam Jaffer Idd, ameiambia Raia Mwema kuwa mechi si nyepesi kama watu wanavyofikiri, maana mabao 2-1 waliyoshinda mchezo uliopita si ya kuridhika kwani BYC ni timu nzuri na ana hakika wanataka kusonga mbele kutokana na faida ya bao moja walilopata nyumbani kwao.
“Mechi siyo rahisi kama watu wanavyofikiri, lazima tuwe makini na tunashukuru wachezaji wanajua jukumu lao kuwa watanzania wote wanawatazama wao.
“Tunashukuru Serikali inatuunga mkono pamoja na TFF walileta mwakilishi wao Mzee Mshangama ambae tulikuwa nae wakati tunawapokea wageni wetu mpaka tunawafikisha hoteli ya Safaya Court Ltd tukisindikizwa na Polisi, inata moyo sana, iliyobaki watanzania waje kwa wingi ili kushangilia kwa nguvu kuhakikisha tunashinda mchezo huu,” alisema Jaffer.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 37 wakiwemo wachezaji 21 umeongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.
Benchi la ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Robert Lartey akisaidiwa na Samuel Sumo wakati Meneja wa timu ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.
Azam FC na BYC wanakutana katika mchezo wamarudiano utakaochezwa siku ya jumamosi Aprili 6 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Azam wanashuka dimbani wakiwa kifua mbele baada ya kushinda katika mchezo wa awali uliochezwa mjini Monrovia katika uwanja wa ATS kwa mabao 2-1.
Endapo Azam watashinda mchezo huo wataingia katika hatua ya tatu ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), ambapo watakutana na timu kutoka Morocco au Libya.

0 comments:
Post a Comment