- Yadaiwa ni kutafuta ushahidi, mipango yakwama
MPAMBANO
wa chini kwa chini wa kudhibiti moto wa udini unaotishia umoja wa Taifa
umeanza, vyombo vya usalama vikiingia kazini kwa kujichomeka kwenye
makundi ya harakati za kidini ili hatimaye kuuzima moto huo, Raia Mwema,
limeelezwa.
Matukio hayo yanatokea katika wakati ambao, nchini hakuna sheria rasmi wala si Katiba ya nchi, inayoweka masharti ya uchinjaji wanyama lakini nchi ikiwa katika utamaduni wa muda mrefu watu wa dini moja kati ya Waislamu na Wakristo, kuvumilia wa dini nyingine kuchinja wanyama, hasa katika shughuli zinazojumuisha watu wa dini zote.
Hayo yakiendelea Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Machi, mwaka huu, amekemea tena vitendo vya udini akisisitiza umoja miongoni mwa Watanzania bila mipaka ya dini zao.
Lakini mbali na Kikwete, baadhi ya viongozi wakuu wa dini mbalimbali nchini wamekwishakutoa wito wa kupata suluhu dhidi ya dalili hizo mbaya zinazoweza kuliangamiza Taifa.
Hata hivyo, wakati hayo yote yakitokea, ikiwa ni pamoja na kauli za kupinga udini zinazobeba tafsiri mbalimbali ambazo ni pamoja na baadhi ya viongozi wa dini kutaka serikali kutoona haya kuheshimu matakwa ya Katiba na sheria za nchi, jijini Mwanza, mapya yaliibuka wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa za uhakika zinabainisha ya kuwa, uongozi wa Parokia ya Kirumba, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, ulifanya uamuzi wa kuchinja ng'ombe na nguruwe, kwa ajili ya kitoweo cha waumini wao wakati wa Pasaka.
Hata hivyo, uamuzi wa uongozi huo wa Parokia hiyo ni kama pia umezua jambo jingine, Raia Mwema likielezwa ya kuwa maofisa kadhaa wa usalama katika siku ya tukio hilo walikuwa wakivinjari eneo husika na kwa namna fulani kusababisha taharuki miongoni mwa wafuasi wa parokia hiyo.
Inadaiwa ya kwamba tangu kutokea kwa tukio hilo, maofisa hao (majina yanahifadhiwa) wamekuwa wakifika kanisani hapo kwa nyakati mbalimbali na kuuliza kuhusu tukio hilo ili kukusanya taarifa zinazoitwa “muhimu”.
Chanzo chetu cha habari kinaeleza ya kuwa Siku ya Jumamosi wiki iliyopita, katika Parokia hiyo ya Kirumba walichinja ng'ombe na nguruwe kwa ajili ya kuuzia waamini wa kanisa hilo kitoweo hicho na kwamba, maofisa usalama walikuwa wanavinjari eneo hilo la Kanisa mpaka kwenye nyumba ya mapadri, huku wakijaribu kutaka kupata ushahidi wa kuwapo kwa tukio hilo la uchinjaji wa kitoweo parokiani hapo.
"Tukiwa tunakatakata nyama alikuja mtu mmoja wa makamo akamwita kijana mmoja mtumikiaji hapa kanisani akataka amuuzie kichwa cha ng'ombe lakini kwa vile hahusiki akamuelekeza kwetu. Alipokuja kwetu tukaanza kupatana naye, baadaye akaja mtu mmoja akatuambia huyu mtu hana na nia njema na hicho kichwa anatafuta ushahidi kwa kazi aliyotumwa," anaeleza mmoja wa waumini waliokuwa wakishughulikia kitoweo hicho.
Kwa mujibu wa kijana huyo, walikubaliana kumuuzia kichwa hicho cha ng'ombe kwa shilingi 15,000, lakini wakati bado akiwa anarandaranda eneo hilo ndipo walipoarifiwa kuhusu dhamira isiyoeleweka ya ofisa huyo na aliporudi kwa ajili ya kuchukua kichwa hicho walimwambia vyote vimekwishakununuliwa.
Inadaiwa ya kuwa baada ya taarifa hiyo kumfikia Paroko wa Parokia ya Kirumba, Padri Francis Mtema, alitoka nje na kumkuta ofisa huyo akizungukia eneo la nyumba ya mapadri akielekea maeneo ya jiko la mapadri ambako haikueleweka alikuwa anatafuta nini na ndipo Paroko alipomwita ofisini kwake.
"Paroko alipomwita walikaa ofisini kwa muda mrefu, zaidi ya nusu saa, sisi tulivyomshtukia tukafuatilia kusikiliza kilichokuwa kikiendelea humo ofisini, na kwa kweli tulikuwa tukihofia usalama wa padri, alipofika alimuuliza kama yeye ni muumini wa parokia hiyo lakini alisikika akisema Misungwi au Mkolani, hatukusikia vizuri, ofisa huyo alikuwa anazungumza kwa sauti ya chini," anasimulia mmoja wa waumini aliyekuwa akimfuatilia ofisa huyu.
Inaelezwa kuwa katika mazungumzo hayo Paroko alimwambia kuwa kama kweli ni mtu wa serikali, basi wao ndiyo tatizo kwa kuwa walivyosikia wamechinja kitoweo hapo wamekwenda kupeleleza, lakini yanapotokea masuala mazito yanayohitaji wana usalama kuyashughulikia kama tishio la waumini na viongozi wa kanisa hawaonekani kuchukua hatua kwa wakati.
"Mimi nilikaa pale mlangoni kwa muda, Paroko alimwambia kama kweli ametumwa, amefuata nini au kuna kosa gani waumini wake kuchinja na kugawana kitoweo kanisani kwao, akahoji kama hilo nalo ni suala zito la mpaka kutumwa ofisa wa usalama kanisani hapo," kilieleza chanzo chetu.
Hata hivyo, Paroko Mtema hakutaka kuzungumzia mazungumzo yake na ofisa huyo kwa maelezo kuwa kama padri hawezi kuweka wazi mazungumzo yake na waumini wake.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa Parokia ya Kirumba imekuwa ikizungukiwa na watu wa usalama kwa muda mrefu ambao inadaiwa ama wamekuwa wakibeba utambulisho kuwa ni waumini wageni wamekwenda kusali au kama madereva teksi wanaopeleka na kusubiri abiria kanisani hapo.
Sababu inayotajwa kwa wana usalama hao kuwepo mara kwa mara katika eneo hilo ni ukweli kwamba mikutano ya kamati ya ulinzi ya umoja wa makanisa ya kikristo mkoani Mwanza imekuwa ikifanyika parokiani hapo.
"Hawajaanza leo, ni siku nyingi tangu tulivyoanza vikao vya umoja wa makanisa, wamekuwa wakija na hata siku ya Alhamisi Kuu, yule ofisa aliyetaka kununua kichwa cha ng'ombe alikuja, tulikaa naye huku nje kwa kuwa watu walikuwa wengi ndani, akanunua baadhi ya vijitabu, akawa ananiuliza maswali, ninaonaje hali ilivyo hapa, uhusiano wetu na dini nyingine. Lakini kwa kuwa ilikuwa katikati ya ibada sikuwa namjali,” alisema kiongozi mmoja wa parokia hiyo.
Baadhi ya waumini wachache waliopata fununu za kuwapo ofisa huyu walionyesha hofu.
"Sasa kama huyu ni ofisa wa serikali na kama ana nia njema, kwa nini aje kwa siri kama suala ni kuchinja nyama hiyo siyo siri watu walitangaziwa kanisani, inawezekana hata asiwe mtu wa serikali," alisema muumini mmoja wa parokia hiyo.
Mivutano ya kuchinja ilianza mwaka jana katika Kijiji cha Buseresere, mkoani Geita, ikiibua mgogoro wa nani mwenye haki ya kuchinja wanyama kwa ajili ya kitoweo kati ya Wakristo na Waislamu wa huko.
Baadaye mivutano hiyo ilimlazimu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kufika mkoani Mwanza kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo ambalo hata hivyo, bado ufumbuzi kamili haujafikiwa ingawa matumaini ya kulimaliza ni makubwa.

RAIA MWEMA
0 comments:
Post a Comment