Dar es Salaam. Watu wawili
wamekufa maji na wengine idadi kama hiyo, kukijeruhiwa katika matukio
tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kionondoni,
Charles Kenyela ,alisema katika mkoa huo, maiti ya mtu mmoja
aliyetambuliwa kuwa ni Magreth Kusupa (35), imekutwa ikiwa inaelea juu
ya maji katika Mto Mbezi.
Alisema maiti huyo alikutwa saa 2:00 asubuhi
katika eneo la Goba na kwamba wananchi wa eneo hilo, walifanya jitihada
za kumopoa.
Alisema “Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mwili wa
marehemu haukuwa na jeraha na umehifadhiwa katika Hospitali ya
Mwananyamala.”Kamanda Kenyela alisema mtu mwingine aliyetambuliwa kuwa
ni Serafini Ameros, mpiga tofali amekufa maji na wenzake wawili, wakiwa
wamejeruhiwa wakati wakijaribu kuokoana kwenye karo lililojaa maji.
Kamanda Kenyela alisema tukio hilo lilitokea saa
8:00 mchana katika eneo la Mbezi Msakuzi wakati Amaros akijaribu
kuondoa uchafu kwenye shimo ambalo lingetumika kama choo.
Alisema shimo hilo liko nyumbani kwa Damian Laurent ambaye katika tukio hilo alijeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment