pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

NGUZO ZA SIMU ZA TTCL KIHESA ZAANGUKA KIHESA NA KUZUA TAHARUKI KUBWA

Mwananchi  mkazi  wa  Kihesa akipita  jirani na nyanya  za  simu zilizoanguka
Nguzo  zaidi ya  mbili  zikiwa  zimeanguka jana  jioni eneo la Kihesa Transfoma
gari  ikipita  kwa shida  eneo  hilo baada ya nyaya kuangukia barabarani
Hili  ndilo eneo ambalo  limekubwa na tatizo la nyaya kuanguka
Mvua  kubwa  zilizoendelea  kunyesha  katika Manispaa ya Iringa juzi na jana  zimeleta  maafa  katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa baada ya  nyumba  moja  eneo la Mlandege  kuanguka na katika  eneo la Kihesa nguzo za  simu  za TTCL kuanguka na kusababisha hali ya taharuki kwa wananchi  wa  eneo hilo la Kihesa Transfoma.

wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wananchi  wa  eneo hilo  wamesema  kuwa  kutokana na tatizo hilo wanaomba uongozi  wa TTCL  kuweza  kufika eneo hilo kunusuru  hali hiyo.


Kwani wamedai  kuwa mbali ya  kuwa chanzo cha nguzo hizo  kuanguka ni mvua  ila inaonyesha nguzo zilizonyingi zimeoza  kupita  kiasi katika  mji  wa Iringa na  kuwa si tukio la kwanza kwa nguzo kuanguka .


Hata hivyo  wametaka TTCL na TANESCO kupita  kuhakiki  nguzo  zao  mitaani ili  kuepusha madhara kwa  binadamu iwapo  nguzo hizo  zitaanguka kama hizo  za TTCL .

0 comments:

Post a Comment