Kijana aliyefahamika kwa jina la Frank Satrun(26)
mkazi wa Mikocheni ambaye ni dereva bajaj afariki dunia baada
ya kugongana na gari aina fuso.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa ajali
hiyo ilitokea barabara ya Mandela eneo la Mabibo hostel,
ambapo gari namba T 439 AUZ aina ya fuso iliyokuwa
ikiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika akitokea ubungo
kuelekea buguruni ndipo alipoigonga kwa nyuma bajaji aina ya
TVS yenye namba T 937 CQL iliyokuwa ikiendeshwa na marehem
Frank na kusababisha kifo chake papo hapo.
Baada ya ajali hiyo maiti ilihifadhiwa hospitali ya
amana huku gari na bajaji vikihifadhiwa kituo kidogo cha
polisi external.
Aidha jeshi la polisi kanda maalum limesema kuwa
hakuna aliyekamatwa na jitihada za kumtafuta dereva
aliyesababisha ajali na kukimbia zikiendelea.

Wakati huo huo eneo la relini barabara ya Kawawa
dereva wa bodaboda aliyefahamika kwajina la Abubakari
Liviga(59) alifariki dunia baada ya kongwa na gari aina ya
Tata.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ajali
hiyo ilisababishwa na dereva wa gari namba T 967 CLQ
iliyokuwa ikiendeshwa na Mkombozi Mrisho Hussen (29) mkazi wa
mtaa wa Ruvuma akitokea veta kuelekea Karume ndipo
alipoigonga kwa nyuma pikipiki namba T 152 CJH aina ya fekoni
iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu Liviga ambao wote walikuwa
na muelekeo mmoja.
Taarifa zinasema kuwa Liviga alikutwa na umauti akiwa
njiani akipelekwa hospitali ya Temeke na maiti imehifadhiwa
hospitalin hapo .
Jeshi la polisi limethibitisha kukamatwa kwa dereva huyo na huku upelelezi ukiendelea
0 comments:
Post a Comment