VIJANA wasiojulikana wanaosadikiwa kuwa wafuasi
wa kundi la ubaya ubaya, wamelishambulia kwa mawe na mapanga gari la Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar.
Hata hivyo, wakati tukio hilo likitokea Katibu
Mkuu Wizara hiyo, Khamis Mussa, hakuwemo.
Tukio hilo
lilitokea majira ya saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Mwanakwerekwe nyumba
mbili ambapo kwa makusudi vijana hao wanaokisiwa kuwa zaidi ya 40 waliizingira
barabara hiyo na kuanza kurusha mawe na kuliharibu gari hilo.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema uwa
sababu ya vijana kufanya hivyo ni kutokana na wafanyakazi wa Baraza la manispaa,kuwazuia
vijana hap wasichimbe mchanga na
kukamatwa ng’ombe wao ambae walikuwa wakimtumia kwa kazi hiyo.
Alisema baada ya ng’ombe wao kuchukuliwa
waliamua kukaa barabarani na kuanza kuzishambulia kwa mawe baadhi ya gari za serikali
na kuliharibu hari hilo.
Aidha walisema kuwa vijana hao wanaojulikana
kwa jina la ubaya ubaya wamekuwa wakikatazwa mara kwa mara kuchimba mchanga
lakini hawasikii.
Akizungumza na gazeti hili baada ya tukio hilo
dereva wa gari hilo, Haji Mrisho Ali, alisema gari hilo lilishambuliwa wakati
akienda nyumbani kwa Katibu Mkuu huyo Chukwani, kumchukua mke wa bosi wake.
Aidha alisema wakati akijihami kwa kukwepa mawe
hao, gari hilo lilijigonga na ukuta na kupinduka, hata hivyo hakuna majeraha
aliyopata.
Nae
Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wizara hiyo, Ramadhani Senga Salmini,
alisema, vijana hao wana lengo la kuitia hasara serikali kwa hivyo lazima
washughulikiwe.
Gari hilo
limeharibiwa kwa kuvunja vioo vyote na sehemu nyengine kadhaa.
0 comments:
Post a Comment