Mahakama nchini Ufaransa,
imemhukumu kifungo cha miaka 25 jela jasusi mkuu za zamani wa Rwanda
Pascal Simbikangwa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Simbikangwa alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji hayo na kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.Simbikangwa alikanusha madai hayo.
Haijuikani kama mawakili wa Simbikangwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Simbikangwa,mwenye umri wa miaka 54, anatumia viti vya magurudumu baada ya kuhusika na ajali mwaka 2008 alipokuwa anaishi katika kisiwa cha Mayotte.
Upande wa mashitaka uliitaka mahakama kumfunga jela maisha Simbikangwa, baada ya kumtaja kuwa mtu mkatili na ambaye anaweza kufanya mambo mabaya zaidi ya aliyofanya.
Mawakili wake hata hivyo walisema kuwa kesi hiyo ilishinikizwa zaidi kisiasa na kuwataja mashahidi kama wasioweza kuaminika na ambao walikuwa na chuki wakati wakitoa ushahidi wao.
Takriban watu 800,000 wengi wao wa kabila la Tutsi , waliuawa katika kipindi cha siku miamoja.
bbc
0 comments:
Post a Comment