Na Mwandishi wetu
MGOMBEA wa CUF katika uchaguzi mdogo jimbo la
Chalinze, Fabian
Skauki,amemuwekea pingamizi mgombea wa Chadema, Mathayo Mang’unda Torogey akisema amepoteza sifa ya kuwa
mgombea.
Katika pingamizi yake kwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), mgombea huyo alisema Torongey amejaza taarifa za uongo kwenye
fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni biashara wakati sio kweli kwa sababu
hajaweka vielelezo.
Aidha alisema mgombea huyo alisema anajua kusoma na kuandika kiswahili na
kiingereza, taarifa ambazo ni za uongo na kwamba mgombea huyo hajui kusoma wala
kuandika kiswahili seuze kiingereza, na kwamba amedanganya.
Hoja ya tatu alisema mgombea wa Chadema amedanganya
kwa kughushi saini za wadhamini, ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba
kuthibitishwa kuwa mgombea.
Alisema katika fomu hizo wadhamini wote saini
zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura na kwamba saini zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio
muhusika.
Hoja ya nne alisema mgombea huyo ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya
kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28
ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la Chalinzi na
kwamba taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani, hivyo anabakiwa na
wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Ameiomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa
mgombea huyo kwa kuwa anakosa sifa za kuendelea kuwa mgombea.
zanzinews
0 comments:
Post a Comment