Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kama Bi. Jeanne Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa mbili na nusu asubui wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala kwenda juu.
Bi.
Jeanne na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic
Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia ya Rongai – Kibo –Marangu
safari ambayo ingewachukua siku tano.
Hadi
sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda
kileleni Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na
kuelekea kilele cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii
isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa
hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika
la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours
wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao wanaelekea
eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa
kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa kuna mawingu
mazito katika eneo la mlima.
Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
22.03.2014
0 comments:
Post a Comment