Ngiri
ni Mnyamapori mtukutu huwasumbua wakulima wa mihogo na viazi vitamu
hivyo hulazimika kuwindwa lakini huweza kukimbia kwa kasi kati ya
kilometa 48 kwa saa kwa urefu wa mita 200 mwendo ambao ni wa kasi zaidi
kuliko wanariadha yeyote duniani.
Ngiri
ana pua kubwa,macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi
uliopinda au ulionyooka.Huwa ana mwili mkubwa,miguu mifupi na nywele
zilizojiviringisha.Ana kwato nne kwa kila mguu,mbili ni kubwa za mbele
zikitumika kutembelea.
Ngiri
huweza kuzaa msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropic,lakini hasa
misimu ya mvua.Ngiri jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18
kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika
mimba.Ngiri dume huweza kushiriki maswala ya uzazi katika umri wa miezi 8
mpaka 10.Kwa uzao mmoja,wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12waitwao
vibwagala kasha kuachishwa kunyonya,familia mbili au tatu zinaweza
kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana
0 comments:
Post a Comment