Mtandao wa kijamii wa , Twitter,
unafungwa nchini Uturuki , saa chache baada ya waziri mkuu , Recep
Tayyip Erdogan, kuahidi kuuondoa .
Bwana Erdogan -- ambaye anakabiliwa na kashfa
kubwa ya ufisadi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa
uchaguzi kuwa hajali kuhusu namna jamii ya kimataifa itakavyochukulia
hatua yake .Neelie Kroes, ambaye ni naibu rais wa tume ya muungano wa Ulaya amesema umamuzi wa kufungwa kwa mtandao huo ni wa kulaumiwa .
Serikali ya Bwana Erdogan imekuwa ikilalamika kuwa mtandao wa Twitter ulipuuza uamuzi wa mahakama ulioitaka viunganishi vya taarifa zake vinashukiwa kurekodi mawasiliano yake binafsi.
0 comments:
Post a Comment