pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Anuani za makazi kuanza karibuni

Postamasta Mkuu, Deus Mndeme

SHIRIKA la Posta Tanzania limeanza utekelezaji wa mfumo mpya wa anuani za makazi na postikodi katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Dar es Salaam.
Mfumo huo umelenga kila mwananchi kuwa na anuani kamili inayotambulisha makazi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deus Mndeme, alisema mfumo mpya wa anuani unaweka msukumo na shinikizo katika kutoa huduma mtambuka zinazofikia viwango vya kimataifa.
Alisema mikoa hiyo mitatu ni mfano na kwamba wamepanga kuutekeleza nchi nzima huku akielezea kuwa Dodoma wamefanya katika kata nane, Dar es Salaam tisa, Arusha nane.
tanzania daima

0 comments:

Post a Comment