John
Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na wakati wote kufungiwa
ndani kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi yake
|
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KWANI HATUNA JINSI IMEBIDI TUONYESHE KILA SEHEMU YA MWILI YA MTOTO HUYU KWA MATESO ALIYOKUWA AKIPATA HATA KUKAA ANASHINDWA |
Shangazi huyu ndiye anaetuhumiwa kumtesa mtoto huyu |
Mwanahawa Nassoro[32] mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela. ndiye anaetuhumiwa kumtesa mtoto John Msumba |
Hali ya kiafya ya mtoto huyo si nzuri |
Vidole vimevimba kutokana na vipigo vya mara kwa mara |
Jeraha kubwa juu ya jicho la mtoto huyo kutokana na kipigo toka kwa shangazi yake |
Hiki ndicho chumba alichokuwa anafungiwa mtoto huyo |
Licha ya
Asasi mbalimbali za kijamii kama TAMWA, GBV,TGNP na Dawati la jinsia la Jeshi la
Polisi kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto Mkoani Mbeya
bado vitendo hivyo vimeendelea kushamiri.
Katika
matukio mawili yaliyotokea Jijini Mbeya hivi karibuni yamewakumba watoto wawili
wa wakazi wa Kata za Iyela na Iduda ambao wamejeruhiwa vibaya kwa vipigo na
kuchomwa moto na walezi wao.
Tukio la
kwanza limemhusisha mtoto wa kiume aliyefahamika kwa jina la John
Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na wakati wote kufungiwa ndani
kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi yake aitwaye Mwanahawa Nassoro[32]
mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela.
Vitendo
hivyo vimetokana na kudaiwa mtoto huyo kujisaidia hovyo hali iliyomletea
usumbufu Mwanahawa ambapo mama yake hayupo na Baba mzazi aliyefahamika kwa jina
la Sumba Dinda akiwa machimboni wilaya ya Chunya takribani miezi miwili
iliyopita.
Sakata hilo
lilibainika baada ya kutokea msiba mtaani hapo Machi 12 mwaka huu majira ya saa
nne asubuhi mtoto huyo alipokuwa akilia majirani walisogea eneo la tukio na
kukuta mlango umefungwa kwa kufuli hivyo kumlazimu Mjumbe wa mtaa Bi Rehema
Mohammed kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa huo Enock Mwampagama.
Mwampagama
alitoa taarifa kwa Mtendaji wa mtaa Henry Chaula ambapo walimkamata kwa
mahojiano katika ofisi ya mtaa na baada ya maelezo walimpeleka kituo cha Polisi
Mwanjelwa kwa hatua zaidi.
Uchunguzi
umebaini kuwa mtoto huyo amekuwa akiteswa kwa muda mrefu ingawa majirani na
mwenye nyumba aliyefahamika kwa jina la Ollen Kaguo hawakuweza kutoa taarifa
ili kunusuru afya ya mtoto ambaye ameonekana kuwa na ukosefu wa chakula bora na
mwili ukiwa umejaa majeraha makubwa.
TUKIO LA PILI
Mtoto Anjela Rashid[4]amechomwa moto mikono yote miwili na baba yake mzazi baada ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake huyo |
Inasikitisha sana |
Mtoto amelala bila ya uwangali zi wa mtu yeyote yule |
Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema akihesabu mabati ili yauwze kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo |
Hapa ndipo anapo lala mtoto huyo |
Mabati yakitolewa ili yauzwe zipatikane fedha za matibabu ya mtoto huyo |
Tukio
la pili limetokea machi 8 mwaka
huu mtaa wa Kanda ya juu kata ya Iduda ambapo mtoto Anjela Rashid[4]ameunguzwa
na moto mikono yote miwili baada
ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake.
Mama yake
mzazi wa mtoto huyo hakuwepo wakati wa tukio hilo kutokana na kukimbia kwa
mumewe Rashid Mwatiya[32] ambapo
amekimbilia Sumbawanga Mkoani Rukwa majuma mawili yaliyopita ili kuwepa vipigo
vya mara kwa mara alivyokuwa akipata.
Baada ya
kutenda unyama huo Mwatiya alimfungia mtoto huyo ndani bila kumpatia matibabu
yoyote na chakula kwa hofu ya kukamatwa kutokana na majeraha makubwa mikononi
hali inayomfanya mtoto kushindwa kula chakula kwa kutumia mikono.
Kutokana na
vidonda kutopatiwa matibabu vidole vimeanza kuoza na kutokana na maumivu makali
mtoto amekuwa akilia mara kwa mara ndipo kilio hicho kilibainishwa na Balozi
Shaban Tolinga ambaye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa lakini hakuchukua
hatua zozote huku mikono ya mtoto ikioza.
Hata hivyo
Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema baada ya kupata taarifa ya ukatili huo
aliamua kufuatilia akiwa na waandishi wa habari ambapo mtoto alikuwa amelala
sebuleni bila uangalizi wowote na njaa hali ilyomlazimu Mtendaji kuchukua
mabati manne kuyauza ili kumpatia matibabu na chakula na kuhakikisha mtuhumiwa
anakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Kwa upande
wake Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Iduda amesema vitendo vya kikatili katika
Kata yake vimekuwa vikifumbiwa macho kwa hofu ya kujenga uadui kwa watu
wanaotoa ushahidi.
Aidha Afisa
Ustawi wa Jamii Mkoa amesema vitendo vya kiatili havita vumiliwa hivyo wananchi
watoe ushirikiano ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekithiri kwa siku za
hivi karibuni.
Na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment