ukizungumzia
foleni mkazi wa Dar es Salaam atakuelewa haraka sana kuliko mtu mwingine kwa sababu
hili ndo tatizo ambalo kila mtu linamgusa jijini, hii ni kwa wote wanaotumia
usafiri binfsi (private transport) na wale wanaotumia usafiri wa umma (public
transport), katika makala yangu hii nitazungumzia sababu kuu 10 zinazosababisha
foleni jijini,
SABABU
KUU 10 ZINAZOSABABISHA FOLENI JIJINI DAR ES SALAAM
1.
1. UTUNZAJI
MBOVU WA MIUNDO MBINU YA BARABARA
Hii
inaweza ikaonekana kama si sababu miongoni mwa sababu zinazosababisha foleni
jijini, ukizungumzia miundo mbinu ya barabara unaongelea vitu kam, mifuniko ya
chemba barabarani, vibao vya kuonesha alama za barabara, madaraja na vyuma
vyake, mitaro ya barabarani, pamoja na Macalvat, utanzaji mbovu wa vitu hivi
umesababisha foleni kuongezeka, wananchi wamejihusisha na biashara ya vyuma
chakavu inayosababisha kuibiwa kwa mifuniko barabarani, pia vyuma vya madaraja,
mifuniko ikiibiwa magari lazima yatapungunza speed sehemu yenye shimo kulikwepa
hivo kusababisha foleni, pengine magari kutumia njia moja kwa kusubiriana jambo
linaloongeza foleni, hii imechangiwa sana na umaskini wa wananchi
2.
UCHONGAJI
NA UBUNIFU MBOVU WA BARABARA
Barabara
nyingi jijini zimetengenezwa kwa fikra ya kupita magari tu, pegine ilikuwa ni
kwa ajili ya magari adogo ya abiria, barabara hizi hazijazingatia watembea kwa
miguu, waendesha baskeli na wale watumiaji wa Pikipiki na Bajaj. Utumiaji wa
barabara moja kwa matumizi ya watu tofauti unasababisha msongamano mkubwa wa
magari barabarani, hii ni kutokana na kile unachoweza kuita upeo mdogo wa
mamlaka zilizo husika katika ujenzi wa barabara hizo
3.
BARABARA
ZA CHINI YA KIWANGO
Barabara
nyingi jijini zina mashimo, hii ni kutokana na utengenezaji wake uliokuwa chini
ya kiwango, hali hii inasababisha magari mengi kushindwa kutembea katika mwendo
wake uliopangwa, magari mengi yanatembea mwendo wa kawaida sana katika baadhi
ya maeneo kutokana na maeneo yale kukumbwa na mashimo ya kupindukia, Mfano
barabara ya kwa remy sinza kupitia tandale ni moja ya barabara ambayo ina
mashimo mengi
4.
ONGEZEKO
LA KUMILIKI MAGARI KWA WATU WA DAR ES SALAAM
Watu
wengi wa Dar es Salaam waanamiliki magari kulinganisha na mikoa mingine
kitakwimu, magari yanaongezeka lakini bado miundombinu ya barabara haiongezeki
hii ina kuwa haiwezi kutengeneza uwiano sawa kati ya magari yaliyopo na
barabara za kupit a magari hayo, familia moja inaweza kumiliki magari 3 magari
yote hayo yatoke asubuhi, hapohapo familia zaidi ya 100,000 za aina hiyo
zifanye kitu hicho hicho kuelekea sehemu moja, hii itapelekea idadi ya magari
300,000 sehemu moja
5.
MCHANGANYIKO
WA VYOMBO VYA USAFIRI BARABARANI
Barabara
zetu hazijatengwa kutumiwa kwa aina tofauti za vyombo vya usafiri, mchanganyiko
katiika matumizi unasababisha sana foleni, mfano unakuta GUTA liko katikati ya
magari, mkokoteni humo humo, hii inasababish amagari yashindwe kutembea katika
mwendo unaostahili, kwa sababu speed ya
GUTA na ile ya gari ziko tofauti lakini gari linalazimika kutumia speed
ileile ya guta kuepusha ajali
6 AJALI
Aajili
ni moja kati ya sababu kubwa inayosababish afoleni katika baadhi ya maeneo
jijiini, katika takwimu ajali zote za nchini 75% ni zile zilizotokea Dar es
Salaam, Pindi itokeapo ajali magari mengi husimama kupisha uuchunguzi wa ajali
hiyo barabarani na hata kama ajali hiyo itasogezwa nje kidogo ya barabara
lakinin hutumia mda mrefu sana kufanya hivyo kitu ambacho husababish
amsongamano mkubwa wa magari
7
UJENZI
MBAYA WA VITUO VYA MABASI
Vituo
vingi vya mabasi havijajengwa kumudu magari mengi, pia vituo hivi vimeingia
sana barabarani, kitendo kinachosababish ausumbufu kwa watu wanaotumia magari
binafsi, magari ya abiria yapopaki barabarani sehemu nyingine ya magari hubaki
barabarani inayo wazuia watu wengine kuendelea na safari zao, hii husababisha
makelele mengi ya honi na kusababisha foleni kubwa barabarani
Itaendelea
………
0 comments:
Post a Comment