KAMPUNI ya Hamadombe Distributor inayomiliki kundi la sanaa la
Hamadombe, imetangaza kutoa dau nono kwa yeyote atakayemkamata
mtengenezaji ama muuzaji wa CD bandia za filamu ya ‘Yote ni Baba’ iliyo
sokoni kwa sasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, muigizaji wa kundi hilo Mary
Joseph ‘Vanessao’, alisema kuwa kampuni yao imeamua kutangaza hivyo ili
kudhibiti wimbi la hujuma za kazi zao, ambazo wamekuwa wakitumia
gharama kubwa kuziandaa, lakini wanaonufaika ni watu wengine.
“Hamadombe inasimamia kazi zake na imetangaza dau hilo, kwa sababu
haioni kazi inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Chama
cha Haki Miliki Tanzania (Cosota), ambapo licha ya filamu nyingi kuwa
na stika ya TRA, lakini bado zinatengenezwa feki na kuingizwa sokoni,”
alisema Vanessa.
Alisema kuwa wasanii wote wa kundi hilo huwa wanasambaza wenyewe
filamu zinazotengenezwa na Hamadombe Distributor na hutumia pia mwanya
huo kuwasaka watu ambao wanafanya mchezo huo mchafu.
Msanii huyo aliwataka pia wasanii wa makundi mengine kupendana ili
kudhibiti wimbi hili, kwani serikali imeshindwa kuwasaidia, hivyo ni
vema wao wakawa kitu kimoja kusaka kazi feki na kuziondoa sokoni na kwa
kufanya hivyo watafanikiwa.
freemedia
0 comments:
Post a Comment