pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

BA APELEKA CHELSEA NUSU FAINALI, MADRID YAPITA KWENYE TUNDU LA SINDANO

BAO la dakika ya 88 la Demba Ba limeivusha Chelsea hadi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla 3-3, usiku huu ikishinda 2-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London. 
Andre Schurrle alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 32, akimalizia pasi ya David Luiz na baada ya hapo PSG wakawabana The Blues hadi dakika za lala salama Ba alipofanya vitu.
Shujaa; Demba Ba ameonyesha thamani yake kwa Jose Mourinho
Jose Mourinho alikuwa mwenye furaha kubwa leo baada ya bao Ba
Kocha Jose Mourinho ambaye timu yake ilifungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza mjini Paris, Ufaransa alipagawa kwa furaha baada ya bao la Ba akaenda kushangilia na wachezaji wake kwenye kibendera. 
Ronaldo alikuwa benchi leo kwa sababu ya maumivu
Katika mchezo mwingine, Real Madrid imefuzu kwenye tundu la sindano kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Borrusia Dortmund usiku huu Uwanja wa Signal-Iduna-Park mjini Dortmund.
Mabao ya Marco Reus dakika ya 24 na 37 yaliwafanya wenyeji waende kupumzika wanaongoza kwa 2-0 na kufanya matokeo ya jumla yawe 3-2 baada ya kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza. 

0 comments:

Post a Comment