Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Flava Godfrey Tumaini Maarufu kwa jina la DUDU BAYA / MAMBA ameingia kwenye List ya wahalifu wanaotafutwa na jeshi la polisi jijini Mwanza,
Taarifa
hiyo imekuja baada ya kusemekana kuwa eti juzi alidhihirisha kuwa yeye
ni DuduBaya baada ya kumvamia mama yake mkubwa na kumkata sikio lake,
Akisimulia mkasa huo Mdogo wake Dudu tumbo moja anayeitwa MUETA amesema
Juzi majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza DuduBaya alienda kwa mama
yake mkubwa ambaye alikua anaumwa sana kutokana na uzee,
Dudu alipofika pale alimuita mama yake mkubwa na
hakuitikiwa ndipo alipomkokota mama yake mkubwa kutoka kibarazani nje na
kumuingiza ndani sebuleni akamlaza kwenye kochi na kuanza kumkata sikio
lakini hakufanikiwa kuling’oa lote kwasababu mama mkubwa alipiga kelele
kuita majirani ndipo Dudubaya akatoka nje na kutokomea kusikojulikana,
lakini wakati Dudu anafanya yote hayo mule ndani alikuwepo mtoto mmoja
mdogo ambaye hakuweza kumzuia mjomba wake asifanye ukatili huo,
Majirani wakafika na kutoa msaada wa kwanza kwa bi Mkubwa na kumwahisha Hospitali ya Sekeu Toure akashonwa sikio, kwani sikio hilo halikukatika kabisa kwa sababu kisu alichokua anatumia Dudubaya kilikua butu,
Kwa Mujibu wa Mdogo wa Dudubaya “Mueta” anasema eti Dudu anamtuhumu mama yake mkubwa kuwa ni mchawi na anamroga.
Tukio hili limeripotiwa polisi na DuduBaya anatafutwa na polisi kwa Udi na Uvumba.
0 comments:
Post a Comment