pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Hivi ndivyo Sugua Gaga, Selebuka zilivoapagawisha ‘Kitchen Gala Party’

MWISHONI mwa wiki wanawake mbalimbali waliofurika kuhudhuria kongamano la ‘Kitchen Gala Party’ Ukumbi wa Diamond Jubilee, walijikuta wakishindwa kuvumilia na kuinuka kwenye viti vyao baada ya wasanii Sara Kaisi ‘Shah’ na Mwasiti Almas walipoimba vibao vya ‘Sugua Gaga’ na ‘Selebuka’.
Wasanii hao ambao walipanda jukwaani majira ya saa 11:00 jioni, walijikuta wakiwapandisha mzuka wanawake hao kutokana na ujumbe ambao unapatika kupitia nyimbo zao hizo.
Moja ya mambo yanayovutia kwenye wimbo wa ‘Sugua Gaga’ ya Shah, ni kutokana na kupigwa katika mahadhi ya mduara na maneno yake yakiwa yanawalenga watu wanaoishi maisha ya uswahilini.
Wakati kwa upande wa Mwasiti, wimbo wake wa ‘Selebuka’ umejaa ujumbe unaoelezea wanawake wanaoteseka katika mapenzi, mada ambazo ndizo hasa zilikuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
Hata hivyo, katika burudani hizo Shah alionekana kumfunika zaidi Mwasiti kutokana na kutoa shoo ya uhakika aliyoambatana na wanenguaji wake na kusugua gaga ipasavyo.
Akizungumza na Tanzania Daima iliyotaka kujua nini siri ya mafanikio yake ya kuweza kuimba huku akinengua kwa wakati mmoja, Shah alisema ni mazoezi tu ndiyo yanayomsaidia na kumweka hivyo alivyo.
Kongamano la ‘Kitchen Gala Party’ liliandaliwa na Kampuni ya …. kwa ushirikiano wa Shirika lisilo la kiserikali la PSI-Tanzania.

0 comments:

Post a Comment