pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Kutana na mzee wa ajabu anaye jifunika majivu ya moto kipindi cha baridi kali usiku

Ludvik Dolezal 
 Mzee mmoja ambaye hakuwa na mahali pa kuishi amekutwa akilala katika majivu ya moto kipindi cha baridi kali nyakati za usiku ili kupata joto,
imetokea mzee huyo kuwa na uso uliojaa mavumbi na macho ya kutisha kutokana na tabia yake hiyo
mzee huyo aliyefahamika kwa jina la Ludvik Dolezal kila siku alikuwa akilala kwenye majivu ili kuweza kupona kutokana na baridi kali la Ulaya

"Nalala na nguo zangu katika majivu ya moto, na najifunika na majivu ili kupata joto, nahisi kama niko peponi, nilikuwa na godoro lakini nililichoma moto" alisema mzee huyo

"mda mwingine watu wananisaidia kwa kunipa nguo zaoo zilizo chakaa ili nichome moto nipate joto" aliongeza
Dolezal inasemakana ana uchizi wa akili ambapo unamfanya achome kila alichonacho, lakini ujinga wake wa kujifunika na majivu unamuokoa na baridi kali kipindi cha usiku huko jamhuri ya watu Czech
Dolezal anapokea kiasi cha 280,500/= kwa mwezi kutoka katika msaada wa serikali. kila siku anavuta sigara pakiti moja na akiahidi kutoacha kuvuta sigara kamwe

0 comments:

Post a Comment