pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Maalim Muhidin Gurumo afariki dunia

GURUMO

Waislam husema "Inna Lillah Wainna Ilayh Rajiuun"
Nguli wa muziki wa dansi hapa nchini na aliekuwa kiongozi wa bendi ya msondo ngoma,maalim muhidin gurumo amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

maalim gurumo amefikwa na mauti hayo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa kipindi kirefu,hali iliyompelekea kushindwa kabisa kuonekana tena jukwaani.

msiba upo nyumbani kwa marehemu tabata makuburi na mipango yote itafanyika hapo.

globu ya jamii kwa masikitiko makubwa,inatoa pole kwa wafiwa wote pamoja na wapenzi wote wa bendi ya msondo ngoma mahala popote pale walipo.

tunamuombea kwa mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu maalim gurumo mahala pema peponi.
 
- AMIN.

0 comments:

Post a Comment