JUMLA ya Walimu 298 wa shule za msingi na sekondari walioajiriwa
mwaka huu Wilayani Igunga mkoani Tabora, wameendelea na mgomo wa kubaki
katika na kulazimika kulala katika viti na meza katika ukumbi wa
Halmashauri hiyo siku nne mfululizo wakishinikiza serikali ya Wilaya ya
Igunga kuwalipa mishahara yao.
Wakizungumza na FikraPevu leo Jumatatu Juni 16, 2014 baadhi yao
wakiwa na watoto wachanga wamelalamikia maisha magumu wanayolazimika
kuishi kwa kuomba omba kufuatia serikali ya Wilaya kushindwa kuwalipa
mishahara yao tangu mwezi Aprili mwaka huu, na serikali ya Wilaya hiyo
kuwa na kauli tata kwa kile wanachodai ni kuwadanganya kuwa wangewalipa
fedha zao Juni 13, mwaka huu agizo ambalo uongozi wa Wilaya hiyo lakini
leo wanadaiwa kulitupilia mbali.
Aidha, wamesema tamko lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Rustica Turuka kuwa wangelipwa fedha kutokana na mapato yatokanayo na
makusanyo ya Halmashauri hiyo, lakini leo wamelitupilia mbali tamko hilo
kwa kuwapiga danadana kuwa fedha hazitoki katikahalmashauri hiyo bali
zinatoka hazina.
Baadhi ya waalimu hao, Joseph Ndonga, amesema wamekubaliana kwa
pamoja na kusisitiza kuwa wataendelea kuishi katika ukumbi wa
halmashauri hadi malipo yao yatakapofanyika, kwani baadhi yao
wamefukuzwa kwenye nyumba zo walizopanga kutokana na kushindwa kulipa
kodi ya nyumba.
“Hapa tulipo ni siku ya nne kuanzia Ijumaa Juni 13, 2014,
tutaendelea kuwabana hadi watupe hela zetu kwamaana sisi maeneo
tunayoishi tunakabiliwa na ukata wa hela umekopa unajua mwisho wa mwezi
unapata hela lakini hadi sasa hawasikilizi kilio chetu tumeitwa na DED
kuwa tukubali kupokea shilingi laki moja tumeikataa kwamaana sio hela
tunayodai” alisema Ndonga
Kaimu Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo, Fredi Mhecho, amesema kuwa
sababu ya kucheleweshwa malipo ya waalimu hao ni zoezi la kuhakiki
majina kuendeshwa kwa awamu na kuanzia Aprili hadi mwezi huu zoezi hilo
bado linaendelea na hadi sasa bado wanajaribu kuangalia namna ya kutatua
tatizo hilo.
Polisi wazingira eneo walilopo walimu
Katika hali ya kushangaza walimu hao wamedai kuzungukwa na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mjini humo, hali ambayo imetajwa kuwafanya baadhi ya walimu hao kuingiwa na hofu baada ya kusimamia msimamo wa kutoondoka katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Katika hali ya kushangaza walimu hao wamedai kuzungukwa na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mjini humo, hali ambayo imetajwa kuwafanya baadhi ya walimu hao kuingiwa na hofu baada ya kusimamia msimamo wa kutoondoka katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
“Wakuu wa idara wamepiga simu Polisi kuomba msaada ili waweze
kutuondoa hapa gari la Polisi liko hapa na polisi wa Kikosi Kutuliza
ghasia (FFU) wapo na mabomu ya machozi wakiwa wanazunguka katika maeneo
tuliyopo” alikaririwa mmoja wa walimu hao.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Susan Kaganda, amesema “Hakuna
Polisi waliopo katika ukumbi wa Halmashauri, ninachojua waalimu wapo
pale tangu Ijumaa hadi leo lakini kwa upande wa Polisi kuwepo katika
hilo eneo hakuna”.
Tafiti zinaonyesha kuwa, walimu wa shule za msingi na sekondari
mkoani humo wakati mwingine hulazimika kuacha kufundisha kutokana na
tatizo la ukosefu wa maji kiasi cha kuwalazimu kwenda kutafuta huduma
hiyo kwa muda mrefu bila kuingia darasani.
0 comments:
Post a Comment