Kuna
sheria mpya inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Senet ambayo
sheria hiyo itawaruhusu watoto kuanzia miaka 10 kupewa mipira ya kondomu
na dawa za kupanga uzazi.
Sheria
ya afya ya uzazi ya mwaka 2014 ambayo tayari ipo mbele ya Senet,
inasema kuwa elimu kwa watoto kuhusu afya ya uzazi na ngono wapewe
watoto pengine hata bila ya wazazi kutoa idhini.
Sheria
hiyo imewasilishwa na Seneta mteule Bi.Judith Sijeny anayesema kwenye
pendekezo la mswada huo kuwa watoto wanaovunja ungo wapewe nafasi
yakutosha kupata habari kamilifu kuhusu elimu ya ngono na huduma za
kisiri ikiwa ni pamoja na habari za kutosha na orodha ya dawa za kupanga
uzazi na habari kuhusu ujauzito na uzazi wa mpango.
Muswada
huo unaashiria kwamba wanaovunja ungo ni walio kati ya umri wa miaka 10
na 17 ambao ni wanafunzi kati ya darasa la tano na kidato cha tatu.
0 comments:
Post a Comment