MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi.
Mtuhumiwa huyo, William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi
alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
wilaya hiyo, Faustine Kishenyi.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyango aliieleza
mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 4 mwaka huu
saa 9 alasiri huko Mlezi, Ukerewe.
Katika hati ya mashitaka imeelezwa kuwa mshitakiwa huyo alikutwa
akitenda kosa hilo katika banda la mbuzi nyumbani kwao na mmoja wa
wanafamilia.
Katika maelezo hayo, Onyango alisema mwanafamilia huyo ambaye ni
mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mlezi, baada ya
kushuhudia tukio hilo alikwenda kutoa taarifa kwa baba yao, Maxmilian
Stephan aliyefika na kumkuta mtuhumiwa akiendelea `kuhangaika’ na mbuzi
huyo.
Akifafanua, alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa la
kujamiiana kifungu namba K/F 154 (1) na (2) C sura ya 16 ya marekebisho
ya sheria ya mwaka 2002. Mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na
amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.
0 comments:
Post a Comment