Maafisa wa uchaguzi nchini
Afghanistan wanajiandaa kuhesabu kura zote millioni nane zilizopigwa
katika uchaguzi wa urais wa awamu ya pili.
Ni miongoni mwa makubaliano yalioafikiwa na
waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ili kumaliza
mgogoro wa kisiasa kati ya Wagombea wawili Ashraf Ghani na Abdullah
Abdullah kufuatia madai ya udanganyifu katika shughuli hiyo.Masanduku ya kupiga kura kutoka mikoani yatasafirishwa hadi katika mji mkuu na vikosi vinavyoongozwa na NATO na kulindwa na vikosi vya kimataifa pamoja na wanajeshi wa Afghanistan.
Ukaguzi huo unalenga kutatua mgogoro huo wa kisiasa wakati ambapo wanajeshi wa Marekani wanaondoka nchini humo.
Vilevile utatoa fursa kwa mshindi kubuni serikali ya umoja wa kitaifa.
0 comments:
Post a Comment