Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma
Sayyid Ali Khamenei amesema Marekani na Uingereza zinaunga mkono hujuma
zinazoendelea za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko
Ghaza. Akizungumza Jumamosi usiku mjini Tehran, Kiongozi Muadhamu
amesema nchi hizo mbili si tu kuwa hazijali kuhusu hujuma za Israel huko
Ghaza bali pia zinaunga mkono rasmi hujuma hizo ambazo zimepelekea
Wapalestina zaidi ya 150 kupoteza maisha, aghalabu yao wakiwa ni
wanawake na watoto wasio na hatia. Kiongozi Muadhamu pia amesema katika
dunia ya leo, madola makubwa ya kibeberu yanaunga mkono kila aina ya
uovu na ufisadi maadamu ni kwa maslahi yao na kwamba mkabala wa hilo
madola hayo yanapinga na kukabiliana kinyama na kikatili na kila
utakasifu na utukufu ambao unaenda kinyume na maslahi yao. Ayatullah
Khamenei ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika mkesha wa kukumbuka
siku ya kuzaliwa Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hassan Mujtaba AS.
Kikao hicho kilihudhuriwa na kundi la wahadhiri wa lugha na fasihi ya
kifarsi, malenga wakongwe na vijana hapa Iran pamoja na kundi la malenga
wanaozungumza lugha ya Kifarsi kutoka Afghanistan, Tajikistan, Pakistan
na India. Kiongozi Muadhamu sambamba na kutoa salamu za pongezi kwa
mnasaba huo mtukufu ameashiria hali ya kusikitisha katika dunia ya leo
na kuhoji, je, kwa kuzingatia kuwa malenga wana uwezo wa kudiriki,
kufahamu wana majukumu gani ya kutekeleza kuhusu matukio na hali ya sasa
duniani? Katika kujibu swali hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu amesema kutokana na uwezo walio nao, malenga wanapaswa
kuwasaidia wanaodhulumiwa sambamba na kubainisha haki na ukweli kupitia
mashairi yao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amewanasihi
Waislamu kutumia vyema fursa inayojitokeza katika nyusiku za Laylatul
Qadr katika Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
crd, iran swahili radio
0 comments:
Post a Comment