Utawala haramu wa Israel umeendeleza mashambulizi yake ya kinyama
dhidi ya raia wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza ambapo asubuhi ya leo
umeshambulia kwa makombora mazito eneo la Shujaiya na kuwaua shahidi
Wapalestina kadhaa wakiwemo watoto 2. Utawala wa Kizayuni kwa mara ya
kwanza umetumia ndege zake mpya za kivita aina ya F-18 na F-22 kwenye
hujuma hiyo ambapo nyumba nyingi za Wapalestina pia zimeharibiwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto (UNICEF)
limelaani mauaji ya watoto wadogo huko Gaza na kuitaka Israel kukomesha
mara moja mashambulizi kwenye maeneo ya raia. Utawala ghasibu wa Israel
umetishia kupanua zaidi mashambulizi yake ya nchi kavu ingawa
wanamapambano wa HAMAS wamesema hatua kama hiyo itakuwa ni sawa na
Wazayuni kujitia kitanzi. Hii ni katika hali ambayo, tayari wapiganaji
wa HAMAS wamewaangamiza wanajeshi 15 wa Kizayuni na kuchukua ngawira
silaha zao za kisasa
0 comments:
Post a Comment