Rais Abdul-Fattah al-Sisi wa Misri ametangaza siku tatu za
maombolezo ya kitaifa kufuatia kuuawa wanajeshi 31 kwenye mpaka wa nchi
hiyo na ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu
wa Israel. Maafisa wa serikali ya Misri wanasema matakfiri waliokuwa na
silaha waliwafyatulia risasi wanajeshi hao katika mkoa wa Wadi el-Gedid
ambapo mbali na 31 kuuawa, wengine 5 pia walijeruhiwa. Rais al-Sisi
ameagiza bendera ya taifa ipeperushwe nusu mlingoti kuanzia leo Jumapili
hadi Jumanne jioni. Akitoa agizo hilo, kiongozi huyo ameahidi kutumia
uwezo wake wote kuwafuatilia na kuwakamata wale waliotekeleza mauaji
hayo.
Misri imekuwa ikishuhudia machafuko na ghasia tokea Julai mwaka jana
wakati rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Misri, Mohammad Morsi
alipoondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na
rais wa sasa Abdel Fattah el Sisi ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa
jeshi.
0 comments:
Post a Comment