MAUSTADH jijini Dar es Salaam wamefikia uamuzi
mzito wa kutembeza bakora kwenye vijiwe korofi vya warembo
wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili almaarufu kama
machangudoa au machangu kwa kile kilichodaiwa kuwa wanasafisha jiji
kutokana na kero za vishawishi vya kuharibiwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani.
Kwa mujibu wa sosi aliyewasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers, maustadh hao walianza oparesheni yao waliyoibatiza
jina la ‘Safisha Jiji’ maeneo ya Sinza kwenye mitaa ya Shule ya Msingi
ya Mapambano na jirani na msikiti uliopo maeneo ya Afrika Sana.
Wakati maustadh hao wakiwafungia kazi na kutembeza bakora, OFM
ilifika maeneo hayo na kufanikiwa kunasa tukio zima ambapo iliwashuhudia
warembo hao waliokuwa wakijiuza kwa madai ya kusaka fedha za sikukuu,
wakipewa kibano cha kutosha.
Wakizungumza na OFM baada ya sakata hilo, maustadh hao walisema
wamechoshwa na uchafu unaofanyika kwenye makazi yao huku wakifunguka
kuwa mara kadhaa wanaporudi nyumbani wakitokea msikitini, machangu hao
huwang’ang’ania wakiwashawishi kufanya nao ngono bila kujua wapo katika
mfungo.
“Tumechoshwa na ufuska, mbaya zaidi hawa machangu wanafikia hatua ya
kutung’ang’ania wakitulazimisha tuwanunue bila kujali kama tunatoka
msikitini kuswali,” alisema mmoja wa maustadh hao na kuongeza kuwa
wanauheshimu mwezi huu mtukufu ndiyo maana wameamua kutembeza bakora kwa
machangu hao.
Warembo hao walishuhudiwa wakiwaomba msamaha maustadh hao na kudai
kuwa wamekoma, hawatarudia tena kuwasumbua maustadh.“Jamani kaka zangu
nawaomba msinichape sana nina ujauzito, naomba mnichape kwenye makalio
nimekoma sitarudia tena,” alisema mmoja wa machangudoa aliyekuwa
akitembezewa kichapo.
0 comments:
Post a Comment