Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa
alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25
mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu
kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na
ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko
Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila alivyoitwa na Askofu Mokiwa
ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty
International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la
dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda mfupi baada ya kikao kuanza,
Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka
wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti. Baadae Askofu
Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie kuwakagua kina Mtikila baada
ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo
zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali
zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, “Mlalamikiwa
alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe
na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola,
hakuna aliyebisha.”
Alisema kisha akaendelea “Mshtakiwa
(Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini
kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa
makalio ya mlalamikaji”.
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara zaidi ya kitendo hicho ni
pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata
shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila
anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.
Credit, Gumzo
0 comments:
Post a Comment