Wanamapambano wa Palestina wamewaangamiza wanajeshi 15 wa utawala
wa Kizayuni wa Israel katika mapigano yaliyojiri Jumamosi katika Ukanda
wa Ghaza. Televisheni ya Al Aqsa imeripoti kuwa katika mapigano hayo
vifaru viwili vya kisasa kabisa vya jeshi la Israel vinavyojulikana kama
Merkava vimeharibiwa kabisa kwa makombora ya wapiganaji wa Harakati ya
Mapambao ya Kiislamu ya Palestina Hamas ambao pia wamefanikiwa kuchukua
ngawira idadi kubwa ya silaha za wanajeshi hao wa Kizayuni. Taarifa
iliyotolewa na Brigedi ya Ezzedine al Qassam, tawi la kijeshi la Hamas
imesema wapiganaji wake pia wameharibu magari matatu ya deraya ya jeshi
la Kizayuni. Imedokezwa kuwa makomando wa Hamas walikuwa wamevalia sare
za jeshi la Wazayuni wakati walipotekeleza oparesheni hiyo.
Wakati huo huo utawala wa Kizayuni umeendeleza hujuma zake za kinyama
dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza ambapo jana
usiku Wapalestina wanne waliuawa shahidi. Hadi sasa Wapalestina zaidi
ya 350 wameuawa shahidi na wengine 2,300 kujeruhiwa tokea uanze uvamizi
wa angani na baadaye nchi kavu dhidi ya Ghaza Julai 8. Umoja wa Mataifa
umetangaza kuwa asilimia 80 ya waliopoteza maisha katika hujuma za
Israel huko Ghaza ni raia wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto
wachanga.
0 comments:
Post a Comment