
Umoja wa Mataifa na Marekani zimetangaza kuwa, Harakati ya
Kiislamu ya Palestina Hamas na utawala pandikizi wa Kizayuni wa Israel,
zimekubali kusitisha mapigano kwa muda wa masaa 72, kuanzia asubuhi ya
leo Ijumaa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amenukuliwa
akisema kuwa, kuanzia leo asubuhi kwa nyakati za eneo la Ghaza, kutaanza
kusitishwa vita na kisha Wazayuni na Wapalestina watakwenda mjini
Cairo, Misri kwa minajili ya kuanza mazungumzo. Hata hivyo akizungumza
kwa pamoja na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kerry
amesema kuwa katika kipindi hicho cha usitishaji vita askari wa Kizayuni
walioko katika maeneo ya vita wataendelea kubakia katika maeneo hayo.
Aidha ripoti hiyo imesisitiza kuwa, ni lazima kuchungwa kikamilifu haki
za raia katika kipindi hicho. Kwa mara kadhaa pande mbili zimekuwa
zikiweka makubaliano ya usitishaji vita, hata hivyo utawala wa Kizayuni
umekuwa ukivunja makubaliano hayo kwa kutumia kwa visingizio tofauti na
kuanza kushambulia kikatili maeneo ya raia katika Ukanda wa Ghaza.
0 comments:
Post a Comment