Na Saidi Mkabakuli
Katika kutekeleza mkakati wa
kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vitengo vya mawasiliano serikalini, Mkurugenzi
wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene leo ametembelea Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pia kuzungumza na Mtendaji Mkuu
wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango.
Akiwa katika ziara hiyo, Bw.
Mwambene ambaye ndiye Msimamizi Mkuu masuala ya Mawasiliano Serikalini na
Msemaji wa Serikali amesema kuwa vitengo vya mawasiliano serikali vina jukumu
kubwa ya kuuelimisha umma wa Watanzania juu ya masuala mbalimbali yanayojiri
kwenye ofisi zao.
Bw. Mwambene ameongeza kuwa
lengo kuu la kuanzishwa kwa vitengo hivyo ni kutoa elimu kwa umma na taarifa
sahihi kwa Watanzania ambao ndiyo waajiri wakuu wa watumishi wa umma nchini,
hivyo watumishi wa vitengo husika hawana budi kukidhi haja za Watanzania kwa
kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati.
“Tumieni utaalamu wenu kwa
kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati Watanzania ili kuweza kutoa suluhu ya
masuala mbalimbali ambayo munaweza kuyajibu,” alisema.
Akizungumza wakati alipokutana
na Msemaji Mkuu wa Serikali, Katibu Mtendaji wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango,
alimpongeza na kumshukuru Bw. Mwambene kwa kutenga muda na kutembelea Tume ya
Mipango, ambayo ndiyo Washauri Wakuu wa Serikali katika menejimenti ya uchumi
na masuala ya maendeleo.
Dkt. Mpango aliweka bayana
mkakati wa Ofisi yake wa kuwafikia Watanzania wote bila kujali maeneo yao ya
kijiografia kwa kuwaelimisha juu ya mipango mbalimbali ya serikali yenye
dhamira ya dhati katika kuwavusha katika umaskini miongoni mwao.
“Tuna mkakati wa kuwafikia na
kuwaelimisha Watanzania juu ya masuala ya mipango na maendeleo, na naomba
kuchukua fursa hii kuiomba Ofisi yako kutuunga mkono katika hili ili kuweza
kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV) 2025,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa mujibu wa TDV 2025 ni
kuivusha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
Bw. Assah Mwambene (Kulia) akibadilishana uzoefu na Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi.
Joyce Mkinga (Kushoto) wakati alipotembelea na kukagua Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Katikati) aliyenyanyua mikono akizungumza na
ugeni kutoka Idara ya Habari (Maelezo) walipomtembelea Ofisini kwake. Wanaomsikiliza
ni Mkurugenzi wa
Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kulia) na Afisa Habari wa Idara
hiyo, Bw. Frank Mvungi.
Maafisa wa kutoka Idara ya
Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (Kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi (Kushoto)wakiandika majina yao
mara walipoingia kwenye Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Wapili Kulia) akizungumza na Maafisa
wa kutoka Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (Wapili Kushoto), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na Afisa HabAri wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi (Kushoto) walipomtembelea
Ofisini kwake. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akisisitiza jambo juu ya
umuhimu wa magazeti wakati alipokuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
Bw. Assah Mwambene (Kushoto) akizungumza na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa ziara ya ukaguzi wa
vitengo vya mawasiliano serikali.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akizungumza na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto)
wakati wa ziara ya
ukaguzi wa vitengo vya mawasiliano serikali.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiagana na ugeni kutoka
MAELEZO. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Bw. Assah Mwambene na kushoto
ni Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
Bw. Assah Mwambene (Kushoto) akibalishana kadi za
mawasiliano na Mkuu wa Kitengo cha Maktaba na Nyaraka kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bw. Ally Msovu mara alipotembelea Maktaba hiyo. Kwa mujibu wa taarifa
za ubora wa Maktaba za wizara za serikali hapa nchini, Maktaba hii ya Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango ni ya kipekee na ya kupigiwa mfano na imekuwa ikiwavutia
wageni wengi wa ndani na nje ya nchi wanaoitembelea Ofisi hii.
Picha zote na Saidi Mkabakuli
0 comments:
Post a Comment