
Utawala katili wa Israel umefanya
mauaji ya umati katika mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza
huko Palestina. Taarifa kutoka Gaza zinasema kuwa, Wapalestina 150
wameuawa shahidi kufuatia mashambulio ya Israel katika kipindi cha masaa
24 yaliyopita. Mauaji ya jana na leo ya jeshi la Israel huko Gaza
yametajwa kuwa ni mauaji ya umati. Weledi wa mambo wamezitaja jinai za
utawala wa Kizayuni huko Gaza kuwa ni sawa na jinai zilizotendwa na
Adolph Hitler wa Ujerumani enzi za uhai wake. Miongoni mwa waliouawa
shahidi katika mashambulio ya kinyama ya Isreal wamo wanawake na watoto
wadogo. Wakati huo huo, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa
Kipalestina la Umoja wa Mataifa UNRWA amesema kuwa hali ya kibinadamu
Gaza ni mbaya mno. Wakati ulimwengu mzima ukionesha kusikitishwa na
mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina,
maulama wa Saudia wameendelea kutoa fatuwa za kuwakandamiza Wapalestina.
Abdul Aziz Al Sheikh, Mufti wa Saudi Arabia na Mkuu wa Kamati ya
Maulama wa nchi hiyo amesema kuwa, kufanya maaandamano ya kuwaunga mkono
Wapalestina wa Gaza ni hatua ya kuleta vurugu na isiyo na faida. Kwa
upande wake Swaleh al-Haidan, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mahakama la
Saudia ametoa fatuwa ya kuharamisha maandamano ya kuwaunga mkono
Wapalestina. Al-Haidan ameongeza kuwa, kufanya maandamano ya kuwaunga
mkono Wapalestina ni sawa na kufanya uharibifu katika ardhi.
0 comments:
Post a Comment