BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HELSB), imesema
kuwa itatangaza rasmi majina ya wanafunzi waliokidhi vigezo vya kupata
mkopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa
Elimu na Mawasiliano, Cosmas Mwaisombwa, kwamba mchakato wa upokeaji
maombi kupitia mtandao ulikamilika Julai 31.
“Tumepokea maombi 58,037 na mchakato wa uchambuzi na upangaji wa
mikopo utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya
Vyuo Vikuu nchini (TCU) yatakapowasilishwa rasmi kwenye bodi, kwani
tunategemea taarifa muhimu kutoka kwenye tume hiyo ili kuepuka
udanganyifu,’’alisema.
Mwaisombwa alisema kuwa pia serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi wa
nje waliopata udhamini wa kusoma nchi rafiki na Tanzania ili kuwawezesha
kujikimu.
Aliongeza kuwa malipo ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata, yatakamilika kufikia wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment