WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kuwa daraja la Kigamboni linatarajiwa kukamilika Julai Mwakani.
Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwenye ziara ya
ukaguzi wa miradi inayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Pinda alisema kuwa daraja hilo litasaidia kufungua biashara na
kuongeza mapato serikalini.
Alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60,
ambapo mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa sh. bilioni 117 kati ya bilioni
214 za mradi huo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, alizitaja changamoto
za utekelezaji wa miradi hiyo kuwa ni miundombinu na kueleza kuwa
miradi yote itakamilikwa kwa muda.
Miradi mingine aliyotembelea Pinda ni nyumba za gharama nafuu Mtoni kijichi, na ujenzi wa mji wa kisasa Dege Eco Village.
0 comments:
Post a Comment