Ripoti
iliyotolewa kuhusu tenda ya kuhodhi michuano ya kombe la dunia kwa mwaka
2018 na mwaka 2022 imeelezwa huenda ikasabisha wanaoshutumiwa
kufunguliwa mashtaka
Mbunge wa chama cha Conservative nchini
uingereza, Damian Collins aliitaka ofisi inayochunguza maswala ya
udanganyifu na rushwa kuomba nakala ya ripoti iliyotolewa kuhusu
mchakato wa kutoa tenda kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka
2018 na 2022, akisema kuwa anaamini Ripoti hiyo huenda inatoa ushahidi
kuhusu madai ya vitendo vya rushwa.Mwanasheria kutoka nchini Marekani, Michael Garcia alitoa ripoti yake mwezi huu, lakini Fifa imesema yaliyomo kwenye ripoti hiyo hayatatolewa hadharani
Kamati ya Qatar iliyokuwa ikiwania tenda kuhodhi michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 inakabiliwa na shutuma kuwa ilitoa rushwa kupatiwa nafasi hiyo,baada ya Gazeti moja kuripoti mwezi juni kuwa aliyekuwa makamu wa rais wa fifa Mohamed bin Hammam alitoa rushwa ya pauni milioni tatu ili kupata tenda hiyo.madai ambayo Qatar imeyakanusha.
Uamuzi baada ya kutoka kwa ripoti hiyo utatolewa mwakani.
0 comments:
Post a Comment