pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Msikiti wa Mtambani kizungumkuti kuungua moto tena hapo jana

Msikiti wa Mtambani waungua moto tena 

MSIKITI wa Mtambani, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, umeungua moto tena. Awali msikiti huo uliungua moto Agosti 13, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema chanzo cha moto huo hakijafahamika.
Kamanda Wambura alisema moto huo unasadikika ulianza saa 6:30 mchana katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kike wa kidato cha nne waliowepiga kambi ya kujisomea kwa ajili ya mtihani wa taifa utakaofanyika Novemba mwaka huu.
“Moto huo uliounguza madarasa mwezi uliopita… jeshi la polisi liliiunda timu inayoendelea kuchunguza chanzo cha moto wa awali na hili sasa itabidi tuliweke kwenye uchunguzi,” alisema kamanda Wambura.

0 comments:

Post a Comment