pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Bado tunamchunguza Miss Tanzania 2014 - Basata

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA),
limesema kwamba linaendelea na uchunguzi kuhusu sakata la ushindi wa mrembo wa Tanzania 2014, Sitti Mtemvu na wiki hiiblitakutana na mwandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga. Sitti ameingia katika mzozo na mamlaka za Serikali baada ya kudaiwa kukiuka kanuni za uendeshaji wa mashindano hayo kwa kuwasilisha cheti kinachoonesha umri ulio kinyume cha umri wake halali, jambo ambalo
kwa mujibu wa taratibu za mashindano
hayo, hakupaswa kushiriki. Mshindi huyo wa kitongoji cha Chang’ombe
na kisha Kanda ya Temeke, anadaiwa
kughushi cheti kipya cha kuzaliwa
kilichotolewa Septemba mwaka huu
kinachoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1991, badala ya kile cha awali ambacho kinaoonesha alizaliwa Mei 31, 1989, umri wake sahihi unaomfanya awe na miaka 25. Kwa mujibu wa taratibu za Kamati ya Miss Tanzania, warembo wanaoshiriki shindano hilo hawapaswi kuzidi umri wa miaka 23,
umri ambao tayari kwa mujibu wa vielelezo kadhaa umevukwa na Sitti.
Akizungumza jana kwa simu na gazeti hili, Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Lebejo alisema wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwamba wiki hii watakutana na Lundenga. “Tayari suala hili lipo katika ngazi ya wizara ambao wanaendelea na uchunguzi. Lakini nasi tunaendelea na uchunguzi na wiki hii tutakutana na Bwana Lundenga,” alisemanLebejo na kuongeza: “Kimsingi, tutazungumza kuhusu kanuni na vigezo vyao, maana hao ndio wanaosimamia suala hili
ikiwamo kuchagua majaji. Kwa hiyo,
kimsingi, tunaendelea na uchunguzi na umma utaarifiwa tukimaliza.”
Wakati Basata ikieleza hayo, habari zinadai kuwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), wamekwisha kukifuta cheti kinachotangazwa kupatiwa Sitti, Septemba mwaka huu, kwani si halali kwa mujibu wa vielelezo vyao. Inadaiwa kuwa Rita baada ya kufikia uamuzi huo, imeiarifu Basata ikiitaka ichukue hatua stahiki kwa mrembo huyo ikiwamo kumvua taji hilo, lakini Lebejo alisema jana kuwa wao kama hilo lipo hivyo ni la Rita, kwa sababu wao hawashughuliki na vyeti, bali wakala hao.

0 comments:

Post a Comment