pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Laana: Mtoto achanwa viwembe, vidonda vyawekwa chumvi

wanamshikilia Tausi Omary (30), mkazi wa kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kujeruhi mtoto wa dada yake, Jafari Mashaka (11) kwa kumchanachana mguuni kwa wembe na kisha kuweka chumvi kwenye vidonda, kwa madai ya kumwimbia fedha kiasi cha Sh 4,500.
Mashaka, mwanafunzi wa Memkwa wa
darasa la tatu katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, alikutwa na majanga hayo, majira ya saa 12 ya asubuhi ya Novemba mosi mwaka huu, nyumbani kwao wanakoishi mtaa wa Kiwalani, kata ya Chamwino.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mama mdogo wa Jafari alitiwa nguvuni jana na Polisi kufuatia wasamaria kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiwalani, Salvatory Lipembe , ambaye naye alilifikisha suala hilo Kituo Kikuu cha Polisi cha Morogoro.
Kukamatwa kwa mwanamke huyo,
kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, kupitia Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sophia Ngasso, wa Dawati la kupambana na ukatili wa kijinsia na watoto la Polisi Mkoa. Kamanda alisema baada ya kuwasilishwa kwa taarifa kituoni hapo na Mwenyekiti wa
Serikali za Mtaa, walikwenda kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya kuhojiwa zaidi kuhusu jambo hilo.
Alisema mama mdogo huyo alidai alifanya hivyo baada ya Jafari kuiba Sh 4,500 na ndipo alipompiga kwa fimbo na hatimaye kumchana kwa wembe katika mguu wake kwa sababu ya hasira. Mtoto huyo, akisimulia kisa hicho alidai kuwa kilimkuta majira ya saa 12 asubuhi ya Novemba 2, mwaka huu na kwamba alichuka fedha hizo Sh 4,500 baada ya kuzidiwa na njaa, na ndiyo mama yake mdogo alipogundua alimkamata na kupiga fimbo na baadaye kumchana na kiwembe mguuni, kisha kumtia chumvi.
Alisema, baada ya kukamilisha uchunguzi, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria , ambapo pia alisisitiza
suala la kuheshimika msingi ya sheria na haki za binadamu wakiwemo watoto.

0 comments:

Post a Comment