Timu zilizofuzu kutoka kila kundi ni kama ifuatavyo: Kundi A: Afrika Kusini yenye pointi 12 na Congo pointi 10. Nigeria na Sudan zimetupwa nje.
Kundi B: Algeria na Mali zimesonga mbele kwa alama 15 na 9 kama zinavyofuatana, huku Angola na Lesotho zikifungasha virago.
Kundi C: Gabon na Burkina Faso zimetinga hatua ya fainali kwa kujikusanyia alama 12 na 11 kama zinavyofuatana.
Kundi
D: Cameroon, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zina pointi
14, 10 na 9 kama zilivyoongozana. Sierra Leone imetupwa nje.
Kundi E: Ghana na Guinea kwa alama 11 na 10. Uganda na Togo zimeyaaga mashindano hayo.
Kundi F: Cape Verde na Zambia zenye pointi 12 na 11 zikiziacha timu za Msumbiji na Niger.
Kundi
G: Senegal na Tunisia zina pointi 13 na 14. Misri na Botswana
zimeshindwa kufuzu, pale zilipoambulia pointi 6 na 1 kama
zinavyofuatana. Fainali hizi za Kombe la Mataifa ya Afrika
zinafanyika nchini Equatorial Guinea ambayo nayo imepewa nafasi kutokana
na kuwa nchi mwenyeji wa michuano, baada ya Morocco iliyokuwa imepewa
nafasi ya kuandaa kutaka michuano hiyo kuahirishwa kwa hofu ya ugonjwa
wa Ebola ambao umeziathiri nchi za Afrika Magharibi, hususan Liberia,
Sierra Leone na Guinea. Vigogo wa soka barani Afrika, Nigeria na Misri
hazitaonekana katika fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment