Na
Saidi Mkabakuli, Kyela
Kufuatia
adha ya usafiri wa majini inayowakabili wakazi waishio katika fukwe za Ziwa
Nyasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia kituo chake cha Kyela ipo mbioni
kujenga meli ya abiria na mizigo ili kuwahudumia wakazi hao.
Hayo
yaliwekwa bayana na Mkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema wakati timu
wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango ilipotembelea
na kukagua bandari za Itungi na Kiwira zilizopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Bw.
Ntetema alisema kuwa Mamlaka imeshakamilisha mchakato wa manunuzi na tayari imempata
mkandarasi M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli yenye
uwezo wa kubeba jumla ya tani 200 za mizigo na abiria 200.
“Mamlaka
ipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa mkataba unaotarajiwa kutiwa saini mwezi
ujao na kazi itaanza mwanzoni mwa mwaka
ujao,” alisema.
Bw.
Ntetema aliongeza kuwa mpaka sasa Bandari ya Kyela imeshaanza maandalizi ya
kuvuta umeme uliofadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini pamoja na kuaanza kwa
kujenga matishari mawili ili yaweze kurahisisha utoaji wa huduma mara meli hiyo
itakapoanza kazi mwishoni mwa mwaka ujao.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliupongeza uongozi wa
Mamlaka kwa hatua yake hiyo kwani itaongeza tija ya shughuli za kiuchumi katika
kanda hiyo ya Ziwa Nyasa.
“Ninaupongeza
uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kuanza mchakato huu utakaofungulia fursa za kiuchumi
na maendeleo kwenye ukanda huu, hivyo kuunga mkono jitihada za serikali za
kupunguza vikwazo mbalimbali vinavorudisha kasi ya kusaka kupunguza umaskini
nchini,” alisema.
Bibi
Mwanri aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa za kuhudumia
shehena na abiria kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe, na Ruvuma. Pamoja na kuhudumia
nchi za jirani ikiwemo Malawi, Msumbiji na Zambia.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari
ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili
kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija
katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na
ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda:
Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda
vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo,
mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini
kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.
Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya
rasilimali watu na ujuzi:
Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya
ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika
kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara,
na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa
kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza
idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji
wa huduma za kifedha.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema
akiwakaribishia wakaguzi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema akifafanua jambo kwa Timu ya ukaguzi
wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence (kulia) akihoji masuala mbalimbali yanayohusiana na shughuli za kimaendeleo
zinazofanywa na Bandari ya Kyela.
Kiongozi wa timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence (Mbele) akiwaongoza wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kupanda boti ili kwenda kushuhudia lango
la kuingilia Gati la Bandari ndogo ya Itungi. Itungi ni bandari ya kipekee
nchini kujengwa mtoni.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema
(Kulia) akiwaonesha kitu wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakati wakishuhudia lango la
kuingilia Gati la Bandari ndogo ya Itungi.
Mkuu
wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema
(Aliyevaa tai) akiwaonesha kitu wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo sehemu inapojengwa gati mpya (halionekani) katika Bandari ya Kiwira.
Wajumbe
wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
walipata fursa ya kujionea meli pekee inayotoa huduma ya kusafirisha abiria na
mizigo (MV Songea) katika Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania.
PICHA
ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
0 comments:
Post a Comment