Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani yabshilingi bilioni2.
Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na
mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina
la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi. “Ni kweli tukio la aina hiyo lipo lakini watu
kama hawa siwezi kusema moja kwa moja kuwa Mchungaji ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biasharabhii,” Alisema Nzowa. Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na
Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli wa mambo.
0 comments:
Post a Comment