pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

MSAMA AUCTION MART YAKAMATA MITAMBO, KAZI FEKI ZA MAMILIONI

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama
ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha
Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imekamata kompyuta za kufyatua kazi
feki za wasanii zenye thamani ya mil18. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu pamoja na sapoti ya wasamaria wema.
Alisema kompyuta, mashine na kazi.feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa Kimara Machungwani, jijini Dar es Salaam na
mtuhumiwa huyo amefikishwa katika
kituo cha Polisi kwa ajili ya mchakato
wa kiheria wa kufikishwa mahakamani.

Msama alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi ya wengine.
Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha
mafanikio ya wahusika ambao licha ya
kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu,
wameshindwa kupiga hatua kiuchumi
kutokana na wajanja hao kuingiza kazi
feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya
kutupa.
Msama alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa kushirikiana na
wadau wengine, anashukuru kwamba
kadiri siku zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na
ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa. “Msama Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,” alisema Msama. Aliongeza, kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya wasanii. Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi
hiyo na kazi zenye jumla ya shilingi bil.12.
Msama alisema kampuni yake imejitwika jukumu hilo zito kwa lengo
la kuona wasanii wa Tanzania wananufaika na ubora wa kazi zao
katika kuendesha maisha yao kwamba
kupitia vipaji vyao, wahusika waweze
kujiajiri. Alisema, katika mazingira ya sasa ambapo jasho la wasanii linaishia
mikononi mwa wajanja wachache
ambao wamekuwa wakichakachua kazi, kamwe wasani hawawezi kupata kipato cha kutosha kuboresha maisha yao. Msama ametoa wito pia kwa wasamaria wema sio tu kutoa taarifa kwa kampuni yake au Jeshi la Polisi za kuwafichua wanaojihusisha na uchakachuaji wa kazi za wasanii, pia kuacha kununua kazi feki japo huuzwa kwa bei ya kutupa. Baadhi ya wananchi walioshuhudianbaadhi ya vifaa na kazi feki, kwa nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi hiyonngumu kwa maslahi ya wasanii. Kelvin Living na Iddy Abbas wa Mabibo, kwa nyakati tofauti wameomba kazi hiyo iwe endelevu kwa
sababu wajanja hao wachache wanachangia wasanii kukosa maslahi
mazuri kupitia vipaji vyao.

0 comments:

Post a Comment